UKIONA MWANAUME ANAKUFANYIA MAMBO HAYA BASI JUA UNADANGWA!
(1) Hataki kukupeleka kwake mechi zote mnachezea kwako; Kama una mwanaume anakuambia anakupenda lakini hajawahi kukupeleka kwake, au unapajua kwake lakini hataki muende, ni karibu tu ila anataka kufanyia mapenzi kwako na mara nyingi akija anakula kabisa na kuondoka, anaweza alete matunda au asilete kitu lakini anakula na hata hajiongezi, hataki mchezee kwake kwani inamaanisha ukienda kwake chakula atanunua yeye na si wewe, huyu Dada ni mdangaji jua kuwa unadangwa. (2) Ghafla anafukuzwa au kusimamishwa kazi/biashara haziendi vizuri; Mpaka wakati mwingine unajiona una gundu, umekutana naye hata mwezi haujaisha kasimamshwa kazi, kuna matatizo kazini au biashara imesimama, hujawahi muona kazini wala kuiona hiyo biashara lakini ana maneno maneno mengi kisha anakuomba pesa ya kutumia au akaongezee mtaji, dada yangu mwanaume unayekutana naye ghafla anapata matatizo huyo ni mdangaji unadangwa! Alikua hajawahi kukupeleka kazini, hujaiona Biashara yake lakini ghafla kila kitu kinabadilika. (3) A...