Posts

Hatma ya Kagere Simba Ipo Hivi

Image
  BAADA ya kuenea taarifa kwamba mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere yupo mbioni kutimka klabuni hapo, wakala wa mchezaji huyo, Patrick Gakumba, ameibuka na kufungukia hatma ya mteja wake huyo.   Kagere aliyejiunga Simba msimu wa 2018/19 akitokea Gor Mahia ya Kenya, msimu wa 2020/21 uliomalizika hivi karibuni, alikosa nafasi kubwa ya kucheza kutokana na ushindani wa namba alioupata mbele ya John Bocco na Chris Mugalu.   Akizungumza kwa njia ya simu kutoka nchini Ukraine, wakala huyo alisema: “Tayari Meddie ameongeza mkataba na ataendelea kubaki ndani ya Simba, hivyo watanzania wasitegemee kuwa ataenda kujiunga na klabu nyingine.   “Watu wataendelea kumuona Simba kwani wamemuongezea mkataba japo kwa sasa klabu imeweka maficho sana ila wataliweka wazi baadaye.”Hivi karibuni ilielezwa kwamba, Kagere aliandika barua ya kuomba kuondoka Simba, huku akihusishwa kutakiwa na Yanga

TFF Yamrudisha Kocha wa Simba Bongo

Image
  KAMPUNI ya Afrisoccer kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Kampuni ya La Liga kutoka Hispania, imeandaa kongamano la soka huku aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck akiwa mmoja wa watoa mada. Kongamano hilo limepangwa kufanyika kati ya Machi 18 na 19, mwaka huu litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Maktaba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.   Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mratibu wa Kongamano hilo, Peter Simon, alisema kuwa wadau mbalimbali watashiriki mkutano wenye malengo ya kukuza na kuendelesha soka hapa nchini.   Simon aliwataja walengwa wa Kongamano hilo ni wadau wa soka ambao ni Serikali, Kamati za Michezo za Mikoa na Wilaya, TFF, Bodi ya Ligi Kuu Bara, klabu, Makocha na Mawakala wa Wachezaji. Aidha aliwataja baadhi ya watoa mada katika Kongamano hilo ni Mlamu Mng’ambi (Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba), Senzo Mazingisa (Mshauri wa Yanga), Injinia Hersi Saidi (Makamu Mwenyekiti wa Usajili na Mashindano wa Yanga) na Mar...

Yanga Yaondoshwa Kagame Cup-Michezoni leo

Image
  MICHEZO Y ANGA imeondoshwa   kwenye michuano ya   Kagame Cup baada   ya jana kufungwa   mabao 3-1 na Express katika   mchezo wa mwisho wa   Kundi A kwenye michuano   hiyo. Kuondoshwa kwa Yanga   kunatokana na kushika nafasi   ya tatu katika kundi hilo baada   ya kukusanya pointi mbili   zilizotokana na kucheza mechi   tatu ambapo sare mbili na   kupoteza moja. Express ndiyo   vinara waliokusanya pointi 7,   huku Nyasa Big Bullets ikiwa   nazo tano na Atlabara mbili. Katika mchezo huo   uliochezwa Uwanja wa   Mkapa, Dar, mabao ya   Express yalifungwa na Godfrey   Lwesibaya dakika ya 15,   Muzamiru Mutyaba (dk 37)   na Erick Kenzo (dk 53). Bao   la Yanga lilifungwa na Paul   Godfrey dakika ya 71.

UKIONA MWANAUME ANAKUFANYIA MAMBO HAYA BASI JUA UNADANGWA!

Image
(1) Hataki kukupeleka kwake mechi zote mnachezea kwako; Kama una mwanaume anakuambia anakupenda lakini hajawahi kukupeleka kwake, au unapajua kwake lakini hataki muende, ni karibu tu ila anataka kufanyia mapenzi kwako na mara nyingi akija anakula kabisa na kuondoka, anaweza alete matunda au asilete kitu lakini anakula na hata hajiongezi, hataki mchezee kwake kwani inamaanisha ukienda kwake chakula atanunua yeye na si wewe, huyu Dada ni mdangaji jua kuwa unadangwa. (2) Ghafla anafukuzwa au kusimamishwa kazi/biashara haziendi vizuri; Mpaka wakati mwingine unajiona una gundu, umekutana naye hata mwezi haujaisha kasimamshwa kazi, kuna matatizo kazini au biashara imesimama, hujawahi muona kazini wala kuiona hiyo biashara lakini ana maneno maneno mengi kisha anakuomba pesa ya kutumia au akaongezee mtaji, dada yangu mwanaume unayekutana naye ghafla anapata matatizo huyo ni mdangaji unadangwa! Alikua hajawahi kukupeleka kazini, hujaiona Biashara yake lakini ghafla kila kitu kinabadilika. (3) A...

TOFAUTI KATI YA WANAUME NA WANAWAKE AMBAYO WANAWAKE WENGI HAWAIJUI!

Image
Unapomkosea mwanamke ukawa unamuomba msamaha, anakuambia sitaki, sikutaki, ondoka, akakublock na kutotaka kabisa umtafute basi jua kuwa anahitaji umtafute. Kakublock lakini anataka utafute namba nyingine ili ujaribu kuongea naye, anahitaji utafute rafiki zake, ufanye kila namna ili kumuomba msamaha. Kama ukikaa kimya kwakua kakublock basi mwanamke huumia na ndiyo unaharibu kabisa. Lakini sasa kama umemkosea mwanaume, akakuambia anahitaji muda, akakuambia usimtafute, akakublock, akawa hataki kujibu meseji zako na hataki chochote kuhusu wewe. Ukilogwa ukazidi kumtafuta, ukatafuta na namba nyingine, ukatafuta marafiki zake na kuwaambia matatizo yenu, ukatafuta na ndugu zake ili waongee naye. Ukatuma meseji milioni kuomba msamaha basi jua kuwa ndiyo unaharibu, ndiyo unamuonyesha kuwa huna thamani na huyo mwanaume atakuacha kabisa. Unapomkosea mwanaume fanya juhudi za kumuomba msamaha, mtafute yeye kama yeye, akikuambia umpe muda basi mpe muda kweli. Acha kuhangaika kwa ndugu zake, marafiki...