Yanga Yaondoshwa Kagame Cup-Michezoni leo

YANGA imeondoshwa kwenye michuano ya Kagame Cup baada ya jana kufungwa mabao 3-1 na Express katika mchezo wa mwisho wa Kundi A kwenye michuano hiyo.
Kuondoshwa kwa Yanga kunatokana na kushika nafasi ya tatu katika kundi hilo baada ya kukusanya pointi mbili zilizotokana na kucheza mechi tatu ambapo sare mbili na kupoteza moja.

Express ndiyo vinara waliokusanya pointi 7, huku Nyasa Big Bullets ikiwa nazo tano na Atlabara mbili.Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, mabao ya Express yalifungwa na Godfrey Lwesibaya dakika ya 15, Muzamiru Mutyaba (dk 37) na Erick Kenzo (dk 53). Bao la Yanga lilifungwa na Paul Godfrey dakika ya 71.
Comments
Post a Comment