Posts

Showing posts from August, 2021

Hatma ya Kagere Simba Ipo Hivi

Image
  BAADA ya kuenea taarifa kwamba mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere yupo mbioni kutimka klabuni hapo, wakala wa mchezaji huyo, Patrick Gakumba, ameibuka na kufungukia hatma ya mteja wake huyo.   Kagere aliyejiunga Simba msimu wa 2018/19 akitokea Gor Mahia ya Kenya, msimu wa 2020/21 uliomalizika hivi karibuni, alikosa nafasi kubwa ya kucheza kutokana na ushindani wa namba alioupata mbele ya John Bocco na Chris Mugalu.   Akizungumza kwa njia ya simu kutoka nchini Ukraine, wakala huyo alisema: “Tayari Meddie ameongeza mkataba na ataendelea kubaki ndani ya Simba, hivyo watanzania wasitegemee kuwa ataenda kujiunga na klabu nyingine.   “Watu wataendelea kumuona Simba kwani wamemuongezea mkataba japo kwa sasa klabu imeweka maficho sana ila wataliweka wazi baadaye.”Hivi karibuni ilielezwa kwamba, Kagere aliandika barua ya kuomba kuondoka Simba, huku akihusishwa kutakiwa na Yanga

TFF Yamrudisha Kocha wa Simba Bongo

Image
  KAMPUNI ya Afrisoccer kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Kampuni ya La Liga kutoka Hispania, imeandaa kongamano la soka huku aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck akiwa mmoja wa watoa mada. Kongamano hilo limepangwa kufanyika kati ya Machi 18 na 19, mwaka huu litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Maktaba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.   Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mratibu wa Kongamano hilo, Peter Simon, alisema kuwa wadau mbalimbali watashiriki mkutano wenye malengo ya kukuza na kuendelesha soka hapa nchini.   Simon aliwataja walengwa wa Kongamano hilo ni wadau wa soka ambao ni Serikali, Kamati za Michezo za Mikoa na Wilaya, TFF, Bodi ya Ligi Kuu Bara, klabu, Makocha na Mawakala wa Wachezaji. Aidha aliwataja baadhi ya watoa mada katika Kongamano hilo ni Mlamu Mng’ambi (Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba), Senzo Mazingisa (Mshauri wa Yanga), Injinia Hersi Saidi (Makamu Mwenyekiti wa Usajili na Mashindano wa Yanga) na Mar...

Yanga Yaondoshwa Kagame Cup-Michezoni leo

Image
  MICHEZO Y ANGA imeondoshwa   kwenye michuano ya   Kagame Cup baada   ya jana kufungwa   mabao 3-1 na Express katika   mchezo wa mwisho wa   Kundi A kwenye michuano   hiyo. Kuondoshwa kwa Yanga   kunatokana na kushika nafasi   ya tatu katika kundi hilo baada   ya kukusanya pointi mbili   zilizotokana na kucheza mechi   tatu ambapo sare mbili na   kupoteza moja. Express ndiyo   vinara waliokusanya pointi 7,   huku Nyasa Big Bullets ikiwa   nazo tano na Atlabara mbili. Katika mchezo huo   uliochezwa Uwanja wa   Mkapa, Dar, mabao ya   Express yalifungwa na Godfrey   Lwesibaya dakika ya 15,   Muzamiru Mutyaba (dk 37)   na Erick Kenzo (dk 53). Bao   la Yanga lilifungwa na Paul   Godfrey dakika ya 71.